Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe.Kenani Laban Kihongosi amefika kwenye ofisi za Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha na kupokelewa na Katibu wa CCM mkoa huo Komredi Mussa Dadi Matoroka, leo Julai 01, 2025.
Mhe.Kihongosi licha ya kusaini kitabu cha wageni na kuwashukuru kwa mapokezi makubwa waliyoyafanya na baadaye kufanya mazungumzo mafupi na baadhi ya viongozi wa Chama hicho kwenye kikao cha ndani.
Hata hivyo Katibu wa CCM Komredi Matoroka ametumia wasaa huo kumkaribisha tena Mhe. Kihongosi Mkoani Arusha huku akimshukuru Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kumrejesha tena Arusha kwa kuwa amekuja kuendeleza pale alipoishia alipokiwa mkuu wa wilaya ya Arusha.
Aidha, Matoroka amemuahakikishia kuwa upo ushirikiano mkubwa wa Chama na Serikali kwa ngazi zote katika mkoa huo, hivyo uwepo wake yapo matarajio makubwa ya Chama na Serikali kutoka kwake kama Mkuu mpya wa Mkoa.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa