Serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kutekeleza mkakati wa kuhakikisha huduma za afya zinawafikia wananchi katika maeneo yao hususani wananchi waishio vijijini, lengo likiwa ni kupunguza na kuondoa kabisa vifo vya watoto chini ya miaka mitano pamoja na wajawazito wakati wa kujifungua.
Katika Mkoa wa Arusha, hali ya upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi imeongezeka hadi kufikia asilimia 93 mwaka 2025 kutoka asilimia 65 mwaka 2021, jambo ambalo limewezesha uwepo wa maduka ya dawa ndani ya hospitali, uwepo wa mashine za kisasa katika hospitali zote za Serikali.
Jumla ya Hospitali mpya 8 zimejengwa kataka mkoa wa Arusha, hospitali ambazo zimesheheni vifaa tiba vya kisasa huku Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mount Meru ikiwa na Mashine za CT-Scan, ECHO, ECG na MAMOGRAPHY mashine ambazo hapo awali hazikuwepo kwenye Hospitali za Serikali.
Uwepo wa mashine hizo za kisasa kwa kiasi kikubwa zimepunguza rufaa za wagonjwa kwenda kupata huduma hizo kwenye Hospitali za Rufaa nje ya Mkoa, kama vile KCMC na Muhimbili, kwa sasa wagonjwa wanapata huduma hizo ndani ya mkoa licha ya kuokoa maisha lakini pia imepunguza gharama kubwa kwa wagonjwa.
Hata hivyo historia mpya imeandikwa katika Hospitali ya wilaya ya Karatu @halmashauri_ya_karatu serikali imesimika mitambo ya kuzalishia hewa ya Oksijeni, ambapo awali hewa ya Oksijeni ililazimika kununuliwa kwenye hospitali ya binasfsi, uwepo wa mtambo huo umerahisiha upatikanaji wa Oksijeni kwa wagonjwa wa dharura, katika hospitali zote za mkoa wa Arusha pamoja na mkoa jirani wa Manyara,
Kwa sasa wagonjwa wa rufaa wanaotibiwa ndani ya Mkoa huku idadi wagonjwa 152,332 waliotakiwa kwenda kutibiwa nje ya Mkoa, wametibiwa katika Hospitali ya Mkoa Mount Meru.
Awali, Mkoa wa Arusha umenufaika sana na mkakati wa uborsshaji huduma za afya nchini, kwa kupata fedha za kuboresha miundombinu ya kutolea huduma ya afya kwa kuimarika kwa hali ya utoaji na upatikanaji wa huduma za Afya kwa wagonjwa.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa