MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amewataka wananchi wenye kero au kesi za masuala ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji na ulawiti ambazo hazijapatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu, kufika ofisini kwake Julai 11, 2024 kwaajili ya kufahamu sababu zinazokwamisha kesi hizo na nani anazikwamisha ili kuwezesha wahanga kupata haki zao huku wahusika kupelekwa kwenye vyombo vya sheria
Makonda aliyasema hayo alipokutana na wadau wa Mashirika na Asasi zisizo za Kiserikali, zinazotengeneza faida zinazoshughulika na Maendeleo na huduma za jamii baada ya kuibuka hoja mbalimbali za matukio ya ulawiti na ubakaji ikiwemo mienendo ya kesi zinazopelekwa polisi na mahakamani ikiwemo vituo vya afya.
Amesema kuwa, suala la ubakaji na ulawiti kwa Mkoa wa Arusha limekuwa ni kero kubwa kwa jamii lakini kunabaadhi ya wazazi na walezi hawawajibiki ipasavyo kutokana na wazazi kuwa makini zaidi kutafuta hela na kuwaachia wadada wa kazi majukumu ya familia huku baadhi yao wakilawitiwa na kubakwa kutokana na uangalizi hafifu
"Hizi kesi za ubakaji na ulawiti zinasikitisha sana lakini lazima tutafute kiini chake na kunakesi moja nimeisikiliza na Mkurugenzi wa Husna Foundation, Husna Almasy ametupa uelewa kuwa mama mzazi wa mtoto huyo anajua vema aliyemlawiti mtoto wake lakini anatumia mbinu ya kusingizia watoto wengine kumbe mhusika mkuu anamjua"
Alisema yeye Rc Makonda ni mpole kuliko watu wengine Duniani lakini katika jambo la ulawiti na ubakaji ila ikidhibitika huyu mama anajinufaisha na tukio hili asije kunilaumu nitachukua hatua dhidi ya sakata la mtoto wa miaka mitatu wakiume kufanyiwa ukatili huku mzazi wa mtoto huyo akificha ukweli wa tukio zima.
Alisisitiza kila wazazi na mlezi kusimama imara katika kulinda watoto wasifanyiwe ukatili ikiwemo utaoji wa taarifa ili kufanyiwa kazi na haki ipatikane ikiwemo kuhakikisha maadili yanazingatiwa na ulinzi wa watoto ni jukumu la kila mmoja
Pia aliagiza watu wote waliofanyiwa ukatili kwa watoto kubakwa au kulawitiwa na kesi zao hazijulikani zimeishia wapi wafikie ofisini kwake siku ya alhamisi hii ili waweze kusema ukweli na kujua zimekwama wapi na
Awali mmoja kati ya wadau kutoka Husna Foundation,Husna Almasy alisema si kweli tukio la ulawiti la mtoto wa miaka mitatu kudaiwa kulawitiwa na watoto wenzie Jijini Arusha, si la kweli bali uhalisia wa mtoto huyo kulawitiwa na kesi kushindwa kufikishwa mahakamani kwa madai kuwa waliotenda tukio hilo hawawezi kukabiliwa na kesi ya jinai kutokana na miaka yao kuwa chini ya umri wa kushtakiwa kwa kosa hilo anajua mama mzazi wa mtoto huyo aitwaye Laightness anaujua na vipimo vya daktari zinaonyesha aliyafanya tukio hilo ni mtu mzima na si watoto kama mama anavyodai
Almasy alisema ni kweli watoto walikamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi Murriet lakini uhalisia wa tukio hilo mama mzazi wa mtoto huyo aitwaye Lightness anajua ukweli wa tukio hilo na aliyefanya tukio la ulawiti wa mtoto huyo anamjua lakini hasemi ukweli badala yake anasingizia watoto wanaoishi mitaani
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa