• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

ACHENI KUTATUA KESI ZA UKATILI WA KIJINSIA KIENYEJI- BWANA MOSES MABULA

Posted on: March 23rd, 2022

Watendaji wa Kata na Vijiji wametakiwa kuacha kutatua matukio ya ukatili wa kijinsia kienyeji badala yake wafuate Sheria ili wahusika wachukuliwe hatua kisheria zaidi.

Yamesemwa hayo katika ufunguzi wa kikao cha wadau cha tathimini ya mpango wa Taifa wa udhibiti wa ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto (MTAKUWWA) na Mchumi Mkuu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa bwana Moses Mabula kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa Dkt.Athumani Kihamia.

" Watendaji wa kata na vijiji ndio walinzi wa maeneo yao hivyo ni aibu kama watatua changamoto hizo kienyeji badala ya kufuata Sheria".

Bwana Mabula amesema kikao hicho kiwe chachu ya kupata uzoefu kutoka kwa maafisa maendeleo ya kata ambao wao ndio wanaokutana na wahanga wa matukio hayo ya ukatili wa Kijinsia kwa karibu zaidi.

Aidha, amesisitiza zaidi katika kikao hicho wajumbe hao waibue changamoto zote ili zisaidie kwa ngazi ya Mkoa kupata elimu yakuweza kuipeleka katika halmashauri zingine.

Amesema kwa Halmashauri ya Arusha jumla ya Matukio 4510 yameripitiwa katika vyombo mbalimbali, hivyo Mkoa unahitaji kujifunza zaidi kutoka kwa maafisa hao ili wigo wa utoaji elimu uweze kufika mbali zaidi.

Vilevile amezitaka kamati zote za

 MTAKUWWA ngazi ya Halmashauri na kata kuhakikisha Matukio yanatolewa taarifa katika vituo husika ili kulinda haki za wanawake na watoto.

Nae, mratibu wa mpango wa MTAKUWWA ngazi ya Mkoa Bi. Erena Materu amesema lengo kubwa la kikao hicho ni kufahamu mafanikio na changamoto zilizopo katika ngazi za kata na vijiji na kutafuta mbinu za kuzitatua.

Kuna juhudi kubwa zimefanyika katika kuhakikisha elimu inawafikia walengwa, Afisa ustawi wa Jamii Mkoa bwana Daniel  Kasikiwe amesema jumla ya klabu 625 katika shule ya msingi zimeanzishwa kwa lengo la kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto na klabu 212 katika shule za Sekondari.

Pia, bwana Daniel amesema asilimia 43 ya kamati zimeshapatiwa mafunzo ya namna ya kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto ambacho ni kiwango kidogo sana kwa ngazi ya Mkoa.

Mganga Mkuu wa Mkoa  Dkt. Silvia  Mamkwe amesema athali ni kubwa zinazotokana na ukatili wa kijinsia ikiwemo umaskini kwani wengi wanashindwa kuzalisha na wengine wanakata tamaa ya kuanzisha familia kutokana na madhara wanayokuwa wameyapata.

Dkt.Silvia ametoa wito kwa Jamii kushiriki kupinga ukatili wa kijinsia kwani  ni jukumu la Jamii nzima sio kazi ya polisi na dawati la Jinsia pekee.

Mratibu wa mradi wa familia  kutoka shirika binafsi la SOS bi Erena Mwakalile amesema kupitia mradi huo wameweza kuzisaidia familia nyingi kujikwamua kiuchumi kwa kuwapa elimu na kuwawezesha katika mitaji ili kupunguza ukatili wa kijinsia kwa familia kuwa maskini.

Kikao cha tathimini  cha mpango wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kimefanyika kwa halmashauri ya Arusha chini ya shirika la SOS kwenye mradi wa familia ulioanza mwaka 2008 katika halmashauri hiyo na kushirikisha maafisa maendeleo ya Jamii ngazi ya kata na halmashauri.








Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa