# Kuanzi mwaka 2022 Serikali ilianza mpango wa kuwahamisha kwa hiari wananchi wanaoishi ndani ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Msomera mkoani Tanga.
# Maeneo yaliyotengwa ili kuwawezesha wananchi kuhamia kwa hiari ni Msomera, Kitwai na Sauni.
# Uandikishaji wa wananchi wanaohama kwa hiari kutoka eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Msomera unazingatia haki za binadamu.
# Mpango wa Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanaohama Ngorongoro wanapata huduma bora za kijamii kama walivyo watanzania wengine.
# Mpango wa Serikali ni kujenga nyumba 5000 kati ya hizo 2500 zinajengwa Msomera na 1500 zitajengwa Kitwai na 1000 Sayuni.
# Tangu awamu ya kwanza iliyoanza tarehe 16 Juni, 2022 hadi tarehe 18 Januari, 2023 jumla ya kaya 551 zenye watu 3,010 zilihama ambapo kaya 503 zenye watu 2,692 zilihamia Msomera na kaya 48 zenye watu 318 zilichagua kwenda maeneo mengine. Jumla ya mifugo iliyohamishwa katika awamu hii ilikuwa 15,321.
# Awamu ya pili iliyoanza tarehe 24 Agosti, 2023 hadi 28 Aprili, 2024 kaya 822 zenye watu 5,354 zimehama ambapo kaya 745 zenye watu 4,855 zimehamia Msomera na 77 zenye wayu 499 zimehamia maeneo mengine. Jumla ya mifugo iliyohamishwa ni 21,136.
# Kwa awamu zote mbili jumla ya kaya 1,373 zenye watu 8,364 zimeshahama.
Eneo la Ngorongoro ni maarufu kwa kwa faru weudi duniani.
# Watalii zaidi ya laki saba wametembelea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kati ya Julai 2023 na Aprili 2024.
# Zaidi ya shilingi bilioni mia moja themanini na nane (188.5Bilioni) zimekusanywa kutokakana na ujio wa watalii waliotembelea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.
#Serikali haijasitisha huduma kwa wananchi waliopo katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.
# Wananchi wengi wamehamasika kuhama kwa hiari baada ya kupewa elimu ya umuhimu wa uhifadhi wa eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa