Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ametangaza kuwa Mkoa wa Arusha umeingia makubaliano na Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo kuanzia sasa Mizunguko yote ya barabara (Round about) zilizopo Jijini Arusha zitasimamiwa na Wizara hiyo pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw. Ephraim Mafuru, Mhe. Makonda amesema lengo ni kutumia bustani zilizopo kwenye mizunguko ya barabara katika kuhakikisha kuwa zinakuwa vivutio vya wenyeji, wageni na watalii wanaofika Mkoani hapa pamoja na kuwa jukwaa muhimu la kutangaza mazao mbalimbali ya utalii yanayopatikana Mkoani Arusha.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TTB, amempongeza Mhe. Makonda kwa ubunifu wake akisema utekelezaji wa makubaliano yao na uwepo mikutano mingi ya kitaifa na kimataifa inayofanyika Mkoani Arusha ni sehemu nyingine nzuri ya kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana kwenye Mkoa huu wa Kaskazini mwa Tanzania ulio kitovu cha Utalii kwa Tanzania bara.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa