• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

HALMASHAURI YA ARUSHA YAPONGEZWA

Posted on: June 8th, 2022

Uongozi wa Halmashauri ya Arusha umepongezwa kwa kupata hati safi kupitia taarifa ya Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa miaka mitano mfululizo.

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa, Mkoa wa Arusha,Bi. Susan Mnafe kwa niaba ya Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Dkt. Athumani Kihamia, wakati wa kikao cha kamati ya Fedha Utawala na Mipango, cha kupitia Hoja za Ukaguzi wa Hesabu za  halmashauri ya Arusha kwa mwaka wa fedha 2020/2021.

Licha ya kutoa pongezi hizo, Bi. Susan ametoa maelekezo kwa uongozi wa halmasahuri hiyo, kuhakikisha kabrasha la hoja hizo linafuata muundo na miongozo iliyotolewa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI pamoja na kujaza majedwali hayo kilingana na maelekezo.

Aidha amesisitiza kuweka majibu ya hoja, yakiwa na viambatanisho visivyosababisha maswali, huku hoja nyingine zikiainisha wazi mikakati ya utekelazaji wake, zikionyesha dhahiri kiasi cha fedha kinachohitajika, idadi ya shughuli zitakazotekelezwa kwa mwaka  pamoja na muda halisi wa utekelezaji.

Hata hivyo, Suzan amewasisitiza wataalam hao,  kuhakikisha wanatoa mikopo isiyo na riba kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu sambamba na kufuatilia fedha hizo kurejeshwa kwa wakati kwa kuwa wakurugenzi wote, hupimwa kutokana na uwajibikaji wa mikopo hiyo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani.

Naye, Mkaguzi Mkazi Mkoa wa Arusha, Honest Muya, amewataka wataalamu hao, kuwasilisha majibu ya hoja hizo, kulingana na ushauri uliotolewa na wataalamu kwa kushirikiana na waheshimiwa madiwani ili hoja hizo ziweze kufutwa kabla ya mkutano wa Baraza la Madiwani.

Hata hivyo Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Mheshimiwa Ojung'u Salekwa, amewshukuru wataalamu na waheshimiwa madiwani kwa ushirikiano wao, unaowezesha halmashauri kupata hati safi kwa miaka minne mfululizo,na kuwata wataalamu kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia kanuni, taratibu na miongozo ya serikali, pamoja na kuwasisitiza wataalamu hao, kupokea ushauri uliotolewa na Mkaguzi Mkazi sambamba na kuwasilisha majibu yenye tija ili kufuta hoja zisizo za lazima.

Aidha amemuomba Katibu Tawala kupeleka kilio kikubwa cha halmashauri cha upungufu wa wataalamu hasa katika sekta ya Afya, upungufu unaosababisha baadhi ya zahanati kukamilika majengo na vifaa lakini kushindwa kufunguliwa kutokana na kukosekana kwa wataalamu.

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa