Na Elinipa Lupembe
Jaji Mfawidhi Mahakama ya Kuu Kanda ya Arusha, Mhe. Johachim Tiganga ameongoza wakazi wa Arusha kuzindua maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani Mkoa wa Arusha, iliyofanyika kwenye Soko kuu Arusha leo Juni 01, 2024
Katika maadhimisho hayo, Jaji Mfawidhi amewataka wakazi wa Arusha kufuata sheria za utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa kutumia fursa zilizopo kwa kudhibiti taka ngumu ambazo zinazalishwa kwa kuweka utaratibu wa kuzikusanya kwa muda ambao umekubalika nankuweka utaratibu wa kuziteketeza bila kuleta madhara kwa jamii pamoja na kusimamia matumizi ya nishati safi.
Kilele cha Maadhimisho hayo kinatarajiwa kufanyika Mkoani Dodoma Juni 05, 2024 na mgeni rasmi anataraijwa kuwa Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya wiki ya Usafi wa Mazingira Duniani mwaka 2024 ni Urejeshwaji wa Ardhi, Ustahimilivu wa Hali ya Jangwa na Ukame.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa