• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

KAMATI YA LISHE MKOA WA ARUSHA YATAKIWA KUPANUA WIGO WA KUTOA ELIMU KWA JAMII ILI KUONDOA UDUMAVU KWA WATOTO*...

Posted on: December 15th, 2023

Na Daniel Gitaro


Wajumbe wa Kamati ya Lishe Mkoa wa Arusha wametakiwa kuongeza wigo wa kutoa elimu ya lishe, kwa jamii ili kupunguza idadi ya watoto wenye udumavu, changamoto inayojitokeza zaidi maeneo ya vijijini, katika mkoa huo.


Hayo yamesemwa na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Albano Mussa wakati akifungua kikao cha Lishe Mkoa wa Arusha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa mkoa huo.


Mussa amesema kuwa, licha ya kuwa changamoto ya udumavu kwa watoto inaendelea kupungua siku hadi siku, bado kuna changamoto hiyo kwa watoto wa maeneo ya vijijini,  inayochangiwa na uhaba wa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa lishe kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 2 na miezi 7 hivyo ni vyema wataalam kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kupanua wigo wa kuwafikia wananchi hao.


“Bado mkoa wetu unakabiliwa na changamoto ya utukelezaji wa afua za lishe kutonakana na sababu mbalimbali, hivyo niwatake wataalam kuongeza wigo katika kutoa elimu kwa jamii, zaidi  tukachape kazi kwa bidii ili tuweze kukabiliana na changamoto hii ya udumavu kwa watoto”. Amesisitiza Katibu Tawala huyo.


Sambamba na hayo, amezitaka halmashauri zote za Mkoa huo, kuipa ajenda ya Lishe kipaumbele ikiwa ni pamoja na kupeleka fedha za kutekeleza afua za lishe kwa asilimia 100 kwenye maeneo yao kwa wakati, kama inavyoelekezwa kwenye bajeti zao.


Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Afua za lishe kwa kipindi hicho, Mratibu wa Lishe Mkoa wa Arusha, Doto Milembe, ameahidi kuendelea kupambana na udumavu kwa kuongeza wigo mikakati ya kuendelea kutoa elimu, hasa kwa kinamama wajawazito kupitia vikao mbalimbali, kliniki pamoja na mikutano inayoendeshwa kwenye ngazi ya jamii.


“Tunaendelea kuhamasisha akina mama na jamii yote kwa ujumla juu ya umuhimu wa ulaji wa makundi sita ya vyakula, ili kupata virutubisho vinavyopaswa kwa jamii na watoto pamoja na kuongeza idadi ya milo kwa watoto hadi kufikia milo 5, inayoshauriwa kwa siku”. Amesema Mratibu huyo.


Hata hivyo wadau walioshiriki kikao hicho, wameishukuru Serikali kwa mwamko mkubwa wa kuhimiza umuhimu wa lishe kwa jamii, pamoja na ushirikishwaji wa wadau jambo ambalo linarahisisha kuifikia jamii kwa pamoja kuliko kufanya kazi wenyewe.


Kwa upande wake Sheikh wa Wilaya ya Arusha, Shekhe Hussein Said Ijunje, ambaye amemuwakilisha sheikh wa mkoa huo, licha ya kuwapongeza wataalam kwa kazi wanayoifanya, ameshauri kuongeza nguvu zaidi na kuwafikia wananchi kwenye Kata, Vijiji na Vitongoji na kushirikisha viongozi wa dini, ambao wana ushawishi mkubwa kwenye jamii, kwa ajili ya kufikisha elimu hiyo na kupunguza kiwango cha udumavu kwa watoto wanaoishi maeneo ya vijijini ambapo tatizo ni kubwa kuliko maeneo ya mijini.


Awali, utekelezaji wa afua za lishe Mkoa wa Arusha, unakabiliwa na changamoto za ushiriki mdogo wa wanaume katika malezi, makuzi na lishe ya mtoto pamoja na upungufu wa vifaa vya kufanyia tathimini ya Lishe hususani vibao vya kupimia urefu kwa watoto chini ya miaka 5.



Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa