Wajumbe wa Kamati ya Siasa mkoa wa Arusha, wamemshukuru Mhe. Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na kuwakumbuka wananchi wa kata ya Bwawani, halmashauri ya Arusha, kata iliyopembezoni mwa wilaya ikiwa imepakana na wilaya ya Simanjiro mkoa wa Manyara.
Wajumbe hao, wametoa shukrani hizo za dhati, kufuatia kero kubwa waliyokuwa wanaipata wananchi wa Bawawani ya kukosa huduma za afya jirani na kufuta huduma hizo zaidi ya Km 40 -45, kwenye Jiji la Arusha ama hospitali ya Tengeru yalipo makao makuu ya wilaya ya Arumeru.
Wananchi hao wa kata ya Bwawani wamekiri kuwa Rais Samia amejidhi kiu ya muda mrefu ya kupata kituo cha afya ndani ya kata yao, na kufafanua kuwa uwepo wa kituo hicho licha ya kuokoa maisha yao, utapunguza vifo vya wanawake na watoto wakati wa kujifungu pamoja na kuwapunguzia gharama kubwa na kero ya usafiri walizotumia kusafirisha wagonjwa hususani kipindi cha mvua.
Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa mkoa wa Arusha, Loy Thomas Ole Sabaya, licha ya kuwongeza wananchi wa vijiji vya kata ya Bwawni kuibua mradi huo, kupitia program ya Kaya Masikini, mradi unaotekelzwa na TASAF III, lakini Serikali ya awamu ya sita, imezingatia maombi na kipaumbele cha wananchi na kutoa fedha za kujenga kituo hicho cha afya.
"Niwapongeze wanaBwawani kwa kuibua mradi huumuhimu kwenu na vizazi vijavyo, lakini zaidi tunamshukuru mama Samia kwa umuhimu wa kipekee wa kutoa fedha za kujenga kituoa cha afya, kituo ambacho ni muhimu na maalumu kulingana na Jiografia ya eneo hili la pembezoni, hakika Serikali ya mama Samia ni sikivu, inayojali na kuheshimu mahitaji ya wananchi kisekta" Amebainisha Mwenyekiti Sabaya.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arumeru, Noel Severe, amesema Serikali ya mama Samia, imewakumbuka na kuwajali wananchi wa Bwawani ambao walikuwa kama wametelekezwa kwa miaka ya nyuma.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa