Na. Elinipa Lupembe
Wajumbe wa Kamati ya Siasa mkoa wa Arusha, wametembelea na kukagua mradi wa shule mpya ya Sekondari Lake Eyasi, kijiji cha Laghangareri kata ya Mang'ola, wilaya ya Karatu na kujionea hali ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 - 2025.
Wajumbe wa kamati hiyo wamepongeza kazi nzuri inayofanywa na watalamu, viongozi na wananchi wa kijiji na kata, kwa ushirikiano wao katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kuhakikisha ujenzi wa shule hiyo mpya umekamilika na tayari wanafunzi 124 wamekwishaanza masomo shuleni hapo, kuanzia mwezi Januari 2024.
Hata hivyo, licha ya kuwa mradi huo, umekamilika Mwenyekiti wa CCM mkoa, Loy Thomas Ole Sabaya, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu, kufanyika kwa ukaguzi wa fedha zilizotumika kutekeleza mradi huo, kwa kuwa yupo mzabuni aliyetoa huduma ya mchanga na mawe bado anadai pesa za vifaa hivyo vya ujenzi.
Aidha, ameweka wazi kuwa licha ya changamoto hizo, bado Serikali ya Awamu ya sita inafanya kazi kubwa ya kuhakikisha miundombinu ya kutolea huduma za kijamii, inajengwa maeneo yote nchini na kusogeza huduma karibu na wananchi hususani wananchi waishio maeneo ya vijijini.
"Wananchi wa Mang'ola tunakila sababu ya kuunga mkono juhudi za Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhakiksiha wananchi wanapata huduma karibu na maeneo yao, tunaona zahanati, vituo vya afya zimejengwa, shule, barabara, huduma za umeme zinasambaa vijijini sasa, tuendelee kufanya kazi kwa bidii". Amesema Sabaya.
Shule hiyo ya Sekondari Lake Eyasi, imesajiliwa kwa namba S.6264, imejengwa na Serikali kwa gharama ya shilingi milioni 584.2 kupitia mradi wa kuboresha miundombinu ya shule za sekodnari nchini (SEQUIP)
Kiasi hicho cha fedha, kimejumuisha ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa, jengo la Utawala, Mabara za Masomo ya Sayanzi ya Fizikia, Baiolojia na Kemia, Maktaba, chumba cha TEHAMA, pamoja na vyoo vya wanafunzi.
Awali, wananchi wa Mang'ola wameishukuru serikali ya Awamu ya sita kwa kujenga shule hiyo, ambayo imekidhi haja na matakwa yao, kutokana na watoto wao kuteseka kutembea umbali mrefu kufuata shule za sekondari, uliosababisha watoto utoro na baadhi ya watoto kuacha shule kutoakana sababu mbalimbali ikiwemo mimba za utoto kwa wasichana.
"Tunamshukuru sana Mama Samia, ujenzi wa shule hii, utawawezesha watoto kusoma jirani na nyumbani, jambo ambalo litapunguza utoro na mimba za utotoni, lakini tunategemea watoto wetu kusoma na kupata watalamu watakao litumikia Taifa letu baadaye" Wamesema wananchi wa kijiji hicho cha Laghangareri
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa