Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amefanya ziara ya siku moja ya kukagua miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Karatu.
Katika ziara yake Mhe Mongella amewagiza viongozi wa Wilaya na Halmashauri hiyo kuhakikisha wanasimami miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati na wananchi waanze kupata huduma.
Amesisitiza kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati kutasaidia kuongeza thamani ya miradi hiyo.
Akiwa katika mradi wa Kilimo cha Vitunguu katika Kata ya Mang'ola, Mongella amewaaidi wakulima hao kuwasaidia kuwatafutia masoko ya Vitunguu ya uhakika ili kilimo hicho kiwe cha tija na manufaa kwa wakulima wenyewe na Taifa kwa ujumla.
Amesema Serikali imewekeza fedha nyingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo ili wananchi waweze kupata huduma bora na kwa ukaribi zaidi.
Hivyo, hata wananchi wanatakiwa kuithamini na kuitunza miradi hiyo kwani ni kwaajili ya yao ili wapate huduma muhimu kwa ukaribu zaidi.
Nae, Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Dadi Holace Kolimba amesema wao kama Wilaya wanashirikiania kwa ukaribu sana na viongozi wa Halmashauri ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa haraka kama ilivyopangwa.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Karia Rajabu amesema watayasimamia maelekezo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa ili Halmashauri hiyo iweze kukamilisha miradi yote ya maendeleo kwa wakati.
Katika ziara hiyo Mhe. Mongella amekagua ujenzi wa majengo katika shule ya Sekondari Ayalabe yaliyogharimu Milioni 470 kwa awamu ya kwanza, Ujenzi wa majengo katika Hospitali ya Wilaya ya Karatu yenye thamani ya fedha bilioni 2.4, upandaji na uvunaji wa Vitunguu katika Shamba la Mang'ora na ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje, maabara, jengo la wazazi na upasuaji lililogharimu shilingi Milioni 250 katika kituo cha Afya Mbuga nyekundu.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa