Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda, amefanikisha utatuzi wa mgogoro wa ardhi kati ya wananchi walionunua ardhi kutoka kwa Kampuni ya Green Apartment, shamba ambalo lilikuwa likimilikiwa na Kampuni ya Duluti Estate, wilaya ya Arumeru, kwa kuitaka Kampuni ya Green Apartment kuilipa Kampuni ya Duluti Estate Dola Bilioni 1.4 ili kumaliza mgogoro huo, uliodumu kwa zaidi ya miaka 15.
Mhe. Makonda ametatua mgogoro huo, kufuatia ziara yake ya kikazi ya kusikiliza na kutatua kero na malalamiko ya wananchi, aliyoifanya kwa siku sita kwenye halmashauri za mkoa huo, na wananchi hao kupata fursa ya kuwasilisha lalamiko lao la kudhulumiwa eneo na kampuni hizo, kwenye mkutano uliofanyika eneo la Ngariselo halmashauri ya Meru Mei 29, 2024.
Aidha, baada ya kupokea malalamiko hayo Mhe. Makonda alimuagiza Katibu Tawala mkoa huo, Wanasheria na Watalamu wa Ardhi kukaa na pande zote tatu ili kupat a suluhisho la mgogoro huo ili kila upande uweze kupata haki yake stahiki.
Hata hivyo, Juni 05, 2024 kilikaliwa kikao hicho kilichowakutanisha watalamu wa Serikali kikiongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Albano Musa na pande zote za walalamikaji na walalamikiwa, kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano, Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo na kukubaliana Kampuni ya Duluti Esatate kuilipa Kampuni ya Green Apartment kiasi cha fedha wanazodaiwa ili kampuni ya Duluti Eastate iweze kuhamisha umiliki wa hati ya eneo hilo na wananchi walionunua waweze kupatiwa hati ya maeneo waliyonunua ili kumaliza mgogoro huo.
Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Arusha, Geofrey Mwamsojo, ameelezea mgogoro huo kuwa, ulianza mara baada ya Green Apartment kununua ardhi kutoka kwa Duluti Estate kwa Dola Milioni 2.3 na kulipa fedha za utangulizi Dola 6,000 pekee na baadae kuanza kuuza ardhi hiyo kwa wananchi kinyume na makubalino waliojiwekea kwenye mkataba.
"Kulingana na maazimio ya kikao chetu, Pande zote tatu zimekubaliana kuwa Green Apartment amlipe Duluti Estate Bilioni 1.4 kwanza ndani ya siku 15 na baadaye kumalizia kiasi kilichosalia, huku tukiendelea kufanya taratibu za kukaa Duluti Eastet waanze taratibu za kubadilisha umiliki wa hati ya eneo hilo ili wananchi hao waanze kupatiwa hati zao za umiliki wa ardhi waliyonunua" Amefafanua Kamishna huyo.
Amesema, zaidi ya wananchi 380 walinunua vipande vya ardhi hiyokutokankwa Kampuni ya Green Apartment, na wananchi walishindwa kuendeleza maeneo yao kutokana na kukosa hati za umiliki baada ya Duluti Estate kugoma kutoa hati kuu ya umiliki wa ardhi hiyo kwa Green Apartment kutokana na Kampuni hiyo kutokamilisha malipo ya fedha walizokubaliana kwenye mkataba.
Awali wananchi wa Duluti wamemshukuru Mkuu wao wa Mkoa kwa kazi nzuri anayoifanya ya kurejesha Haki kwa wanyonge, kazi ambayo imektoa mwanga wa kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 15 kati ya Wananchi na Kampuni hizo mbili.
" Tunaishukuru Mhe. Rais mama Samia kwa kutuletea Mhe. Makonda Arusha, amesaidia kutatua kero nyingi za wananchi, sisi tulilipa pesa zetu kununua maeneo lakini hatukuoewa hati, mimi nimelipia zaidi ya miaka 13 tumezungushwa na hatimaye leo tumepata suluhisho". Amesema Josephine Mkunda
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa