Kamati ya ushauri ya Mkoa wa Arusha umepitisha mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya kiasi cha shilingi bilioni 263.2 kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo mishahara ya watumishi na mambo ya maendeleo .
Akifungua kikao hicho mwenyekiti wa kamati hiyo ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema, bajeti hiyo itatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.
Amezitaka halmashauri zote zihakikishe zinasimamia fedha hizo za miradi ya maendeleo kupitia kwa viongozi wa Wilaya na Halmashauri, na hii itasaidia kuondoa hadha kubwa kwa wananchi.
Akisoma taarifa ya mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2019/2020 Katibu Tawala msaidizi mipango na uratibu Moses Mabula amesema bajeti hiyo imezingatia vipaombele mbalimbali vya Mkoa.
Vipaombele hivyo vilivyopendekezwa kwa mwaka 2019/2020 kwa Mkoa wa Arusha ni pamoja na kuongeza uhakika wa chakula na kipato kwa wananchi,kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu kwa kutekeleza mpango wa elimu bure.
Kuboresha huduma za afya kwa kuendelea kujenga vituo vya afya na hospitali za Wilaya,kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kutoka 55% kwa mjini na 70% kwa vijijini,kumalizia miradi yote ambayo hakuisha katika sekta zote.
Pia,kuweka mazingira bora ya uwekezaji katika viwanda,kuboresha sekta ya Utalii kwa utoaji wa huduma bora,kuongeza ukusanyaji wa mapato na udhibiti na kusimamia uchanguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.
Kamati ya ushauri ya Mkoa imekutana kwa lengo kubwa la kupitisha mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka mpya wa fedha 2019/2020 ambao utaanza rasmi Julai 2019 na kipaombele kikuwa ni kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa