• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

MADEREVA WAHUDUMIENI WAMAMA NA WATOTO KWA STAHA

Posted on: June 23rd, 2023

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Uzinduzi wa Mfumo wa Kurahisisha Usafiri wa Dharura kwa Mama Wajawazito na Watoto wachanga wa M- Mama kwa Mkoa wa Arusha uliofanyika katika Hospitali ya Mount Meru.Tarehe 22 Juni 2023.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa madereva wanaoshiriki katika mfumo wa M- mama kuwahudumia akina mama wajawazito pamoja na watoto kwa staha, huruma na upendo pale wanapowasafirisha kutoka katika maeneo mbalimbali kuelekea katika vituo vya afya.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizindua Mfumo wa Kurahisisha Usafiri wa Dharura kwa Mama Wajawazito na Watoto wachanga wa M- Mama kwa Mkoa wa Arusha katika hafla iliofanyika Hospitali ya Mount Meru leo tarehe 22 Juni 2023.

Aidha ametoa rai kwa wale wote wanaohusika na usajili wa akina mama wajawazito kuhakikisha wanatekeleza jukumu hilo kwa ufasaha na kuzingatia namba ya dharura ya simu (115) inafahamika kwa kubandikwa sehemu mbalimbali ili wananchi waweze kuifahamu kirahisi.

Halikadhalika Makamu wa Rais amesema mfumo wa M-mama utakapoenea nchi nzima utawezesha kutimiza malengo ya kitaifa na kimataifa ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vya watoto wachanga huku akihimiza elimu kuendelea kutolewa kwa wananchi kwa kuwahamasisha wanawake wanahudhuria kliniki muda wote wa ujauzito na kujifungua katika vituo vya kutolea huduma ya afya.

Makamu wa Rais amesema serikali itaendelea kuboresha upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga.

Ameongeza kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea na jitihada ya kuongeza idadi ya vituo vya kutolea huduma za Afya vinavyotoa huduma kamili za dharura na upasuaji ambapo hadi kufikia mwaka 2022 Serikali imeongeza vituo vya Afya zaidi ya 500 kutoka vituo vya Afya 155 mwaka 2017/18 pamoja na kuongezeka vituo vinavyotoa huduma za watoto wachanga (NICU) kutoka 14 mwaka 2018 hadi vituo 165 mwaka 2022.

Vilevile Makamu wa Rais amewasihi wakazi wa Arusha pamoja na mikoa mingine kusajili akina mama wajawazito na kutumia mfumo wa M-mama ili kuwanusuru wao pamoja na watoto.

Amesema mfumo huo ni mkombozi mkubwa kwani kwa mkoa wa Arusha tangu uanze kufanya kazi mwezi Aprili 2023 hadi kufikia tarehe 20 Juni 2023 tayari umeshasafirisha jumla ya dharura 607 ambapo Kati ya hizo, asilimia 82 zilikuwa ni dharura za akina mama na asilimia 18 za watoto wachanga.

Makamu wa Rais amesisitiza kuenezwa nchi nzima, Tanzania Bara na Zanzibar utekelezaji wa mfumo wa M- mama na kuwashukuru wadau wa maendeleo wakiwemo USAID, Vodacom Tanzania Foundation na mshirika wake Vodafone Foundation kwa utekelezaji wa Mfumo huo hapa nchini.

Hadi sasa Mfumo wa Kurahisisha Usafiri wa Dharura kwa Mama Wajawazito na Watoto wachanga wa M- Mama unafanya kazi katika Mikoa 16 ya Tanzania Bara (Shinyanga, Lindi, Mtwara, Morogoro, Dodoma, Manyara, Singida, Simiyu, Mwanza, Mara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Mbeya, Songwe na Rukwa) na Mikoa yote 5 ya Zanzibar.

Aidha, Mikoa mingine 10 ya Tanzania Bara ambayo ni Katavi, Kigoma, Tabora, Iringa, Njombe, Ruvuma, Kagera, Geita, Pwani na Dar es salaam ipo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji wa mfumo huo na inatarajiwa kuanza utekelezaji kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa