Kwa kutumia uzoefu mlionao na kwa mafunzo mtakayopatiwa hivi leo, ninaamini mtafanya kazi hii ya kusimamia zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura kwa weledi, bidii na Moyo wa kujituma ili kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa.
Hayo yamesemwa leo na Desemba 4, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli na Ndg. Emmanuel Richard Mpongo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili (2) kwa Watendaji ngazi ya Jimbo, kuhusu uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura.
" Sina shaka kwani kuteuliwa kwenu kumetokana na ujuzi, uwezo na weledi mlionao katika kutekeleza majukumu ya
Kitaifa hivyo ni matarajio ya Tume kuwa elimu hii mtakayopata itawajenga zaidi na kufanya zoezi hili lifanikiwe katika Viwango tarajiwa." amesema Ndg. Richard Mpongo
Aidha, Ndg. Mpongo amewata Watendaji hao kwenda kutoa maelekezo mazuri kwa kuwafundisha waendeshaji wa vifaa vya bayometriki na waandishi Wasaidizi ambao ndio watahusika na zoezi la uandikishaji wa wapiga kura vituoni, huku akiwataka kutoa taarifa mara itakapotokea changamoto ya kiufundi ili itatuliwe haraka na zoezi liendelee.
Akihitimisha, Ndg. Mpongo amesisitiza umakini katika utendaji wa kazi hii muhimu, ikiwemo kuzingatia utunzaji mzuri wa vifaa vya kazi kwa muda wote wa zoezi la uandikishaji.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa