Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango ameiagiza Taasisi ua Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU pamoja na watanzania kwa ujumla kuongeza jitihada katika mapambano dhidi ya Vitendo vya rushwa kwani bado Rushwa ipo na inaminya haki za watanzania wengi.
Akifungua Mkutano wa Mwaka wa TAKUKURU jijini Arusha kwenye ukumbi wa mikutano wa AICC, Makamu wa Rais aliyemuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan, amesisitiza pia kuhusu uadilifu wa Watumishi wa Umma, akisema taarifa nyingi za maadili kwa Viongozi wa umma zimekuwa sio sahihi.
Ameitaka TAKUKURU kufuatilia Nyaraka za mali kwa watumishi wa umma, akisema Kiongozi anapaswa kuwa mtu asiyetiliwa mashaka katika utekelezaji wa majukumu yake kwa umma, akiwataka Maafisa wa TAKUKURU kuwa Viongozi wa kupigiwa mfano katika maadili ya utumishi wa umma na kutoa taarifa za kweli za mali, madeni na jinsi yanavyopatikana kila mwaka.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa