Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amempongeza Mkuu wa Mkoa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda kwa utendaji kazi wake mzuri na kujali maslahi ya wananchi hasa wenye uwezo mdogo kwa Zoezi la Upimaji wa afya kwa kuwaleta madaktari bingwa na wabobezi kwaajili ya kutoa huduma bure.
Dkt. MPango ametoa pongezi leo 04 Juni, 2025 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 55 na Kongamano la Kisayansi la mwaka la Chama cha Wafamasia Tanzania lililofanyika kwenye ukumbi wa kimataifa wa Mikutano (AICC) Arusha ambapo amesisitiza kuwa kazi ya kuwahudumia wananchi ni kazi ya Mungu.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amesema anaendelea kutekeleza kikamilifu Maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wanachi wanyonge na wasio na uwezo wanapata huduma bora ambapo kwa mwaka jana, zaidi ya watu 32.000 walipata huduma ya matibabu ya bure.
Hata hivyo, Mhe. Makonda amewatangazia wananchi wa Mkoa huo uwepo wa kambi ya madaktari bingwa na wabobezi watakaotoa huduma ya matibabu bure kwa Magonjwa yote kuanzia Tarehe 23 hadi 29 Juni mwaka huu.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa