Wachezaji wa timu Taifa ya Mpira wa miguu chini ya miaka 20, wamepatiwa mbinu 3 zitakazo wafanya washinde mashindano ya CECAFA.
Mbinu hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Iddi Kimanta alipowatembelea wachezaji hao katika kambi yao Wilayani Karatu.
Amewaambiwa ili washinde wanatakiwa kuwa na nidhamu kati yao wenyewe, wao na walimu wao na kati yao na wachezaji timu vyingine.
Pili,amesema wanatakiwa kufuata maelekezo wanayopewa na walimu wao na tatu wanatakiwa kupata mahitaji yao mbalimbali ya kujikimu.
Timu ya Taifa ya wavulana chini miaka 20 ipo kambini kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya CECAFA yanayotarajiwa kuanza Novemba 22 hadi Disemba 6,2020 Mkoani Arusha ambapo timu takribani 9 zitashiriki mashindano hayo.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa