Kampuni ya Multicable Limited inayojishughulisha na uzalishaji na usambazaji wa bidhaa za Umeme pamoja na masuala ya utalii imekabidhi Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda pikipiki 10 zenye thamani ya shilingi milioni 30, ikiwa ni muednelezo wa juhudi za Mkuu wa mkoa huyo za kuimarisha Ulinzi na usalama Mkoani Arusha kwa lengo la kukuza sekta ya Utalii .
Akizungumza wakati wa kukabidhi pikipiki hizo, Hussein Ali Bhai kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Kampuni ya MCL Ndugu. Murtaza Ali Bhai, yenye makao yake makuu Jijini Dar Es Salaam ikifanya kazi kwenye majiji yote ya Tanzania bara, kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, mapema leo Mei 25, 2024, wamesema kuwa, wametoa pikipiki hizo kwa ajili ya jeshi laPolisi ili kuimarisha ulinzi na usalama wa watu na mali zao katika mkoa wa Arusha.
Bw. Hussein Bhai amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa juhudi kubwa za kuendelea kuimarisha suala la ulinzi na usalama katika mkoa huo ambao ni nyenzo kuu ya wafanyabiashara na uimara wa uchumi huku wakiahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya awamu ya sita chini ya Jemadari Dkt.Samia Suluhu Hassani pamoja na seriakli ya mkoa wa Arusha eneo ambalo ni kitovu cha Utalii, sekta ambayo inaliingizia Taifa fedha nyingi za kigeni.
"Sisi Multcable Limited tumekuja kuunga juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika kampeni yake ya kuufanya Mkoa kuwa sehemu salama.Tumeona utendaji wake katika kulisaidia Jeshi la Polisi kufanya shughuli zake na tunaahidi kuendelea kushirikiana na Ofisi yake." Ameongeza kusema Bw. Hussein.
Kwa upande wake Mhe. Paul Christian Makonda amesema kukamilika kwa ahadi yake hiyo kwa Jeshi la Polisi ya kuwapatia Jeshi hilo Pikipiki 50 ni muendelezo wa hatua nyingine ya kuwatafutia Pikipiki za Umeme 100 pamoja na magari 20 kwaajili ya kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika jitihada za kuendelea kukuza na kuimarisha utalii na uwekezaji mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Christian Makonda amesema lengo lake ni kuhakikisha Jeshi la Polisi linafanya kazi kwa ufanisi kwa kuwa na vifaa vya kisasa na vya kutosha vitakavyowawezesha kubaini na kuzuia uhalifu na wahalifu kabla haujatokea
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa