Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Jumanne Sagini (Mb) amewataka wananchi kufuata Sheria za Usalama Barabarani ili kuepusha ajali zisisokuwa za lazima
Mhe. Sagini amesema hayo wakati akizungumza na wafiwa ndugu jamaa na marafiki waliofika kwenye chumba cha maiti kwa ajili ya kuwachukua ndugu zao waliofariki kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la Ngaramtoni wilaya ya Arumeru Februari 23, 2024.
Amesema kuwa uchunguza wa awali wa ajli hiyo unaonesha, kuna uzembe mkubwa wa madereva wanaoendesha vyombo vya moto ikiwemo wa magari na bodaboda uliosababisha ajali iliyotekea na kupotewpza masiha ya watanzania na raia wa nje.
Amewataka watanzania wote kuhakikisha wanazingatia sheria za Usalama Barabarani kwa kuwa gari lililobeba mizigo halikuwa na gari dogo la kusindikiza 'escorts' nyuma na mbele lakini eneo lilipokuwa daladala ni eneo la njia panda hivyo si eneo la kupakia na kushusha abiria.
"Wananchi wamelalamikia mwendo kasi wa madereva bodaboda, ninaagiza Jeshi la Polisi kufanya Uchunguzi wa kina na kuona namna ya kuhakikisha vituo vya kupakia na kushuha abiria inakuwa mbali na eneo la njia panda pamoja na kudhibiti mwendo kasi wa madereva wa pikipiko maarufu kama bodaboda" Ameweka wazi Mhe. Sagini
Awali, ameungana na mkuu wa mkoa wa Arusha na viongozi wote wa Serikali pamoja na Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, kutoa pole kwa wafiwa wote na watanzania kwa ujumla, na kuhakikisha maagizo ya Serikali yanafanyiwa kazi.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa