Wanachi wa mkoa wa Arusha jioni ya leo wanatarajia kuungana na wananchi wa Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki kuadhimisha Miaka 25 ya tangu kuanzishwa kwake kwa awamu ya pili mwaka 2000, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda Makonda Rc Paul ameandaa nyama choma kwa ajili ya hafla hiyo muhimu jioni ya leo Novemba 28, 2024.
Tayari wajasiriamali wa chomachoma mkoani humo wameanza maandaliazi huku wananchi wa Arusha wakisubiri kwa hamu hafla hiyo.
Jumuia ya Nchi za Afrika Mashariki kwa mara ya kwanza ilianzishwa mwaka 1967 - 1977 na kipindi cha pili ilianzishwa upya mwaka 200 ikiwa na lengo la kuanzisha soko la pamoja kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Aidha, Jumuia hiyo ina jumla ya Nchi wanachama 8 ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Sudan Kusini na Somalia.
Usipange kukosa, vibela Arusha
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa