• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

MIRADI YA AFYA INAYOJENGWA IENDANE NA THAMANI YA FEDHA.

Posted on: December 13th, 2024

@ortamisemi



Naibu Katibu Mkuu Ofisi Ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Grace Magembe amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri nchini, kuhakikisha wanasimamia thamani ya fedha katika Miradi mbalimbali ya Afya inayotekelezwa katika maeneo yao ili iweze kukamilika kwa wakati na kuwahudumia wananchi kama ilivyokusudiwa.



Dkt. Grace amesema wakati akifungua mafunzo ya mpango wa uwekezaji wa huduma za Afya ya Mama na Mtoto (TMCHIP) yaliyofanyika mkoani Morogoro  yakihusisha Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri, Wahandisi majengo, Maafisa Ugavi, Maafisa Mipango, Wahasibu, PPRA,Waratibu wa Miradi, Makatibu wa Afya na Waganga wafawidhi  kutoka katika mikoa 17 na Halmashauri 25 ambapo mradi  huo umeanza kutekelezwa.



“Kila mtaalamu aliyehudhuria hapa akasimame kwenye nafasi yake, popote pale ambapo mradi utaharibika hakuta kuwa na visingizio hatua stahiki zitachukuliwa kwa sababu wote mpo hapa kama timu moja ya utekelezaji wa mradi huu, hivyo nasisitiza miradi hii ya ujenzi iendane na thamani ya fedha inayotolewa na iishe kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi” Dkt Grace.



Mpango huu wa  uwekezaji kwenye huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto (TMCHIP)  unagharimu zaidi ya dola za kimarekani Mil.275 Kwa ushirikiano kati ya Benki ya Dunia, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Afya Tanzania Bara na Wizara ya Afya Zanzibar.



Mradi huu umejikita katika ujenzi na ukarabati wa vituo vya Afya, ununuzi wa vifaa na vifaa tiba, ajira za watumishi, mafunzo ya watumishi, usimikaji wa mifumo ya TEHAMA na uimarishaji wa huduma za rufaa kwa lengo la  kuboresha huduma za afya na hasa za Uzazi na Mtoto. Huu ni mwendelezo wa jitihada za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vile vya watoto wachanga.


Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa