Naibu Waziri Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Mhe Deogratius Ndejembi amewataka Watendaji wanaosimamia miradi ya TASAF Mkoa wa Arusha kuhakikisha wanakamilisha miradi hiyo ifikapo 31 May mwaka huu.
Mhe Ndejembi aliyasema hayo wakati wa akizungumza na wakuu wa wilaya , wakurugenzi pamoja na watendaji wa Miradi ya TASAF Mkoa wa Arusha ambapo alisema Mkoa huo umepata fedha myingi za kutekeleza miradi hiyo hivyo fedha zilizotolewa zinatakiwa ziendane na miradi itakayotekelezwa ili thamani ya fedha iweze kuonekana na ikamilike kwa wakati .
"Kufikia tarehe 31 may miradi hii iwe imekamilika nikimaanisha majengo yote katika Mkoa huu na mimi naahidi kuja kukagua na kwayeyote atakayeleta mzaha katika matumizi ya fedha za TASAF natoa onyo asifanye, inatakiwa kuwa mzalendo kwa maslahi ya Taifa na kwa wananchi na sio maslahi yako mwenyewe " alisema
Pia Mhe Ndejembi aliwataka waratibu wa miradi hiyo katika halmashauri zote za Mkoa wa Arusha kuhakikisha wanawasilisha miradi hiyo kwa TAKUKURU ili iweze kufuatiliwa kwa ukaribu .
Sambamba na hayo aliwataka waratibu katika Mkoa wa Arusha kuhakikisha wanatafuta namna ya kuokoa fedha hizo kwa kuagiza vitu kwa pamoja , kutumia mafundi wao pamoja na kutumia Force account katoka kutekekeleza miradi hiyo ili iweze kuwa rahisi na kuikamilisha kwa wakati .
"Angalieni namna ya kuokoa fedha kwa kuagiza vitu kwa pamoja hivyo mnavyosema mnatumia wadhabuni mnafanya mambo kucheleweshwa ila mkiungana kama Mkoa na kuagiza vitu vyenu kwa pamoja mtarahisisha kazi itakwenda kwa haraka tutakuwa wakali kweli na sijui kwanini Mkoa mlishindwa kukutana kama halmashauri zote na kuagiza vifaa kwa pamoja "
Kwaupande wake Mwakilishi wa Mkoa wa Arusha ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Said Athumani Mabie aliwataka waratibu pamoja na wahasibu kuhakikisha wanajua vizuri miradi ya TASAF inayotekelezwa katika maeneo yao ili kupata mipango kazi ya kila mradi .
Naye Meneja wa miradi ya muda na fedha kutoka TASAF Paul Kijazi pamoja na Selemani masala ambaye ni meneja malipo kutoka TASAF walisema ili kufikia malengo ni lazima kuwe na timu moja katika kutekeleza miradi hiyo kwa kuwa ni kitu kitakachoweka ufanisi mzuri katika miradi hiyo .
Pia waliongeza kwa kuwataka watendaji kuzingatia maelekezo waliyopewa katika kutekeleza miradi na kuibua ambayo inakuwa ni miradi ambayo ni hitaji la wananchi na kufahamu kuwa Fedha za TASAF ni fedha za Serikali na sio Fedha za TASAF .
Kwaupande wao wakuu wa Wilaya akiwamo Mkuu wa Wilaya ya Longido , Karatu pamoja na Ngorongoro waliahidi kuhakikisha thamani ya fedha hizo inaonekana kwa kutekeleza miradi yenye viwango vikuwa kikao hicho kimewapa njia sahihi ya kwenda kisimamia miradi hiyo .
Wakurugenzi kutoka katika halmashauri mbalimbali za Wilaya katika Mkoa huo walisema kikao hicho ni muhimu kwakuwa kimewapa nguvu ya kwenda kujipanga katika kutekeleza miradi kwa kushirikiana na uongozi wa Wilaya .
Mkoa wa Arusha ulipewa jumla ya shillingi bilioni 3 ambapo unatakiwa kutekeleza miradi 36 ya mradi huo wa TASAF .
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa