Na. Elinipa Lupembe
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Crispin Francis Chalamila akizungumza kwenye Mkutano wa Mwaka wa Viongozi wa TAKUKURU unaofanyika mkoani Arusha, kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha ukumbi wa Lake Nyasa, leo Desemba 16, 2024.
Chalamila ameeleza lengo la Mkutano huo ni pamoja na kufanya tathmini ya utendaji kazi wa TAKUKURU kwa madhumuni ya kuimarisha na kuboresha utendaji kazi, hivyo kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa.
"Viongozi wa TAKUKURU watapata fursa ya kubainisha mafanikio tuliyoyapata kwa mwaka mzima, changamoto zilizotukabili na kubadilishana uzoefu wa namna ya kukabiliana na changamoto, kuweka mikakati jinsi ya kuendelea kushirikiana na wadau wengine, kujipanga vema, kupata mafanikio zaidi ili kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa nchini" Amesema
Aidha, Mkurugenzi Chalamila amebainisha kuwa, Rushwa bado ni tatizo la kidunia, nayotumika kupoka haki ya mtu aliyeistahili na kumpa yule ambaye hakuistahili kutokana na jukumu la kutoa haki amepokea Rushwa na kupindisha sheria.
"Rushwa inawanyima wananchi wengi hasa maskini fursa ya kupata huduma bora za kijamii kutokana na baadhi ya watendaji wasio waaminifu kuzitumia fedha zinazotengwa kuboresha huduma hizo kwa maslahi binafsi"
Hata hivyo Amesisitiza kuwa, Mkutano huo utafanya Tathmini ya yaliyojiri kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba,2024, , ili kuweza kujipanga vema kusimamia haki, kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, kwa uchaguzi Mkuu 2025.
Takukuru Tanzania Ofisi ya Rais - Tamisemi Ofisi ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Kwanza Ikulu habari Zanzibar Makonda Rc Paul
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa