Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 umepitia jumla ya miradi 9 katika halmshauri ya Jiji la Arusha nakuridhishwa na miradi 8 kati ya 9.
Akizungumza katika hitimisho la ziara hiyo Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Bwana Abdalla Kaim ameipongeza halmashauri ya Jiji la Arusha na kuwataka kutekeleza maelekezo yaliyotolewa kwenye miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru mapema.
Mwenge wa Uhuru umepitia jumla ya miradi 9 ikiwemo ya Mazingira, afya, Miundombinu, shule na mradi wa uwezeshaji vijana kiuchumi iliyogharimu zaidi cha sh.bilion 10 na kati yake,mradi 1 iliwekewa jiwe la msingi,mradi 1ulifunguliwa, mradi 1 ulizinduliwa na miradi 6 ilitembelea.
Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Arusha zimekimbizwa katika halmashauri ya Jiji la Arusha na zitaendelea katika halmashauri ya Monduli mnamo Julai 1,2023.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa