Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi nchini Tanzania UVCCM na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa, Mohammed Kawaida Comrade Mohammed Kawaida amefika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda Rc Mkoa Arusha na kumpongeza kwa kazi nzuri katika kuwatumikia wananchi wa Arusha, akimtaja kama miongoni mwa Viongozi wachache wenye maono, ubunifu na wenye kuwaza mbali kwa maslahi ya wananchi wanaowahudumia.
Akitaja baadhi ya matukio yaliyofungua fursa kwa Vijana, Kawaida ameitaja tamasha la Land Rover Festival, Usiku wa Wakuu na wakurugenzi wa Taasisi na mashirika ya Umma pamoja na maadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, pamoja na ukuzaji wa sekta ya Utalii Mkoani Arusha, akisema matukio hayo yamechangia pakubwa kwenye kutoa fursa kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wengi.
"Ukiwa nje huko unaweza kuona kama Mhe. Makonda anacheza, anafanya sherehe na matukio tu, kuwa hakuna anachokifanya lakini ukiliangalia hili kwa kina unaona namna ambavyo uchumi wa Mkoa unapanda, uchumi wa mtu mmoja mmoja unapanda lakini hata Pato la serikali linapanda." Amesema Ndugu Kawaida.
Kwa upande wake Mhe. Makonda amemualika Ndugu Kawaida kwenye sherehe za funga mwaka Jijini Arusha, kuanzia Kesho Disemba 28, 2024 wakati ambapo kutakuwa na tukio la Sanaa ya majukwaani ya The Churchil kwenye ukumbi wa AICC na baadae kufuatiwa na Tamasha la Funga mwaka litakalofanyika kwa siku tatu kuanzia Disemba 29-31 mwaka huu kwenye mitaa mitatu ya katikati ya Jiji la Arusha
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa