*Dkt. BITEKO AWASILI LOLIONDO*
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili mji wa Loliondo wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa kituo cha kurushia matangazo ya TBC Taifa na Bongo FM (Loliondo Ngorongoro) utakaofanyika kesho Aprili 15, 2024.
Mhe. Dkt. Biteko amepokelewa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb), na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bi. Aisha Dachi, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Stephen Kagaigai pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF,) Bi. Justina Mashiba.
#arushafusalukuki
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa