Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Mary Masanja(kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha CPA Ramadhan Madeleka (kulia) pamoja na Rais wa Shirikisho la Mifuko ya Uhifadhi wa Mazingira Barani Afrika Dkt.Theophile Zognou(katikati) toka Cameroon.
Naibu Waziri Masanja yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ambapo leo tarehe 28/08/2023 atakuwa mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa 13 wa Shirikisho la Mifuko ya Uhifadhi wa Mazingira Barani Afrika unaofanyika katika Hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha.
Mkutano huo unajumuisha Mifuko 17 kutoka Nchi 20 za Afrika pamoja na Mifuko rafiki 4 toka Nchi za Bara la Amerika ya Kusini na Karibeni unaanza leo tarehe 28/08/2023 na kumalizika tarehe 01/09/2023.
Sambamba na hilo Naibu Waziri Masanja amesema kuwa Wageni hao mara baada ya kumalizika kwa Mkutano watapata fursa ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo Nchini hususan Mkoani Arusha kwa lengo la kuendelea kutangaza Utalii Duniani kupitia Filamu ya - The Royal Tour iliyoasisiwa na Rais.Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa