Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali pamoja na wananchi wa Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro, mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi kwenye mkoa wa Arusha leo Jumapili Disemba 01, 2024.
Mhe. Rais pamoja na shughuli nyingine akiwa Mkoani Arusha, ameshiriki Mkutano wa 24 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulikwenda sambamba na Maadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya hiyo tangu kuanzishwa kwake kwa awamu ya pili mwaka2000.
Mkutano huo, umewakutanisha Marais na Wawakilishi wao kutoka nchi zote nane za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa