• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RAIS SAMIA AZINDUA HOTEL YA GRAN MELIA

Posted on: November 22nd, 2021
  1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wawekezaji kuwa Tanzania ipo salama dhidi ya maambukizi ya UVIKO 19, hivyo wanakaribishwa kuja kuwekeza zaidi.

Ameyasema hayo alipokuwa akizindua Hoteli yenye hadhi ya nyota 5 ya Gran Melia iliyopo Jijini Arusha.

" Kutokana na hatua tuliochukua ya kutoa chanjo ya UVIKO 19 katika nchi yetu, hatua hii imepelekea kuwekwa miongoni mwa nchi chache zinazoendelea kupambana dhidi ya ugonjwa huu".

Serikali  itaendelea kuhakikisha wawekezaji wanawekewa mazingira mazuri nayakuvutia ili waweze kuwekeza kwa wingi katika nyanja mbalimbali.

Amewashukuru wawekezaji wa hotel hiyo kwa kukubali kuja kuwekeza katika nchi yetu kwani wameweza  kuwekaza kwenye zaidi ya Hoteli 5 ndani ya Tanzania na hivyo kutengeneza ajira nyingi kwa watanzania.

Kuwepo kwa Hoteli hiyo Mkoani Arusha itakuwa ni moja ya kichocheo cha kukuza Utalii ambao ulishuka kwa 59% kati ya mwaka 2019 na 2020 kutokana na janga la ugonjwa wa UVIKO 19.

Hivyo Serikali inaendelea kuhakikisha sekta hiyo ya Utalii inakuwa tena kwa kuwakaribisha wawekezaji zaidi na kuwawekea mazingira rafiki ya uwekezaji kwani ni moja ya sekta inayoingizia Serikali mapato makubwa.

Kutokana na uwekezaji uliofanywa na Hoteli hiyo kwenye sekta ya Utalii ambayo inagusa kila sekta hivyo anatarajia Hoteli hiyo itasaidia kukugua uchumi wa nchi kupitia wakulima  na wavuvi  kwa kutumia zaidi bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi hasa vinywaji ili kuweza kukuza soko la bidhaa hizo na kukuza uchumi wa nchi.

Pia, amezitaka hoteli zote nchini kutumia zaidi vyakula vya kitanzania, ili kudumisha Utamaduni wa Kitanzania.

Waziri wa maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro amemshukuru Rais Samia kwa kuleta uhai mpya kwenye sekta ya Utalii kupitia juhudi anazozifanya za kuitangaza nchi nje ya  nchi, kuleta chanjo ya UVIKO 19 na kuleta ndege 2 upande wa Zanzibar vimekuwa ni miongoni mwa vichochea vya kukuza Utalii nchini.

Amesema  kati ya Januari hadi septemba,2021 Utalii umekuwa kwa asilimia 248 na kuipatia nchi pato kwa asilimia 69 kati ya mwezi Januari na Octoba, 2021ukilinganisha na mwaka uliopita.

Nae, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella amesema takribani asilimia 80 ya watalii wanaoingia nchini hufika Mkoa wa Arusha katika mbuga mbalimbali za wanyama na vituo vingine vya Utalii.

Amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta  chanjo ya UVIKO 19 katika nchi yetu ambayo imeleta hamasa kubwa katika sekta ya Utalii kwani watalii wengi wameweza kuamini nchi yetu ipo salama.

Mhe. Samia Suluhu Hassan amekamilisha ziara yake ya siku ya kwanza Mkoani Arusha kwa kuhudhuria sherehe za utoaji Kamisheni katika chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli na kuzindua rasmi Hoteli ya nyota 5 ya Gran Melia.








Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa