Rais wa Sudan Mhe. Salva Kiir Mayardit, amekuwa Mwenyekiti wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baaaya kupokea kijiti kutoka kwa Rais wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye, ambaye amemalliza muda wake.
Mara baada ya kuchaguliwa, Mhe. Salva Kiiri, amekabidhiwa nyenzo za kufanyia kazi, kwa kipindi chote cha kuiongoza Jumuiya hiyo, nafasi ambayo inadumu kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Hata hivyo Marais wa Jumuiya hiyo, kwa pamoja, wamempongeza kwa kuchaguliwa na kumtakia kila la kheri katika kutekeleza majukumu yake, huku wakimsisitiza kuendeleza na kuimarisha mtangamano muhimu wa nchi hizo, kwa kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi.
Awali, Mkutano wa 23 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya za Afrika Mashariki, umefanyika kwa siku mbili mkoani Arusha, ukitanguliwa na vikao vya ndani na umemalizika jioni ya leo tarehe 24 Novemba, 2023, Ngurdoto wilayani Arumeru.
#eastafricacommunity
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa