• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RAS ARUSHA ASISITIZA UKAMILISHAJI WA MIUNDOMBINU YA UJENZI WA SHULE YA KIUTU.

Posted on: September 1st, 2022


Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Misseile Albano Musa, ametembelea na kukagua maendeleo ya  utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari Kiutu, halmashauri ya Arusha, mradi unaotekelezwa na serikali kupitia program ya kuboresha elimu ya sekondari nchini (SEQUIP).

Katibu Tawala huyo, ameipongeza halmashauri hiyo kwa kutekeleza mradi huo kwa viwango ambavyo ubora wa mradi unaonekana hata kwa macho licha ya kwamba mradi huo bado haujakamilika.

"Ninawapongeza wataalamu wa halmashauri ya Arusha, inaonesha namna gani mnafanyakazi kama timu, endeleeni kufanya hivyo ili kufikia malengo ya serikali ya kuwahudumia wananchi". Amesisitiza Katibu Tawala huyo.

Aidha amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, kuhakikisha mradi huo  unakamilika kwa wakati ili wanafunzi wa kidato cha kwanza wapangiwe shule hiyo na kuanza masomo ifikapo Januari 2023.

Awali akisoma Taarifa ya mradi huo, kwa niaba ya msimamizi wa mardi huo, na Makamu mkuu wa shule ya sekondari Kiutu, Mwl. Upendo Mollel, amesema kuwa mpaka sasa mradi umefikia asilimia 65 kukamilika na makadirio ya gharama za ukamilishaji wa mradi huo ni takribani shilingi milioni 250 fedha ambazo zikipatikana mradi utakamilika mpaka mwisho.

Naye Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, Seleman Msumi, amemshukuru Katibu Tawala huyo kwa kutembelea mradi huo na halmashauri yake kwa ujumla,  na kuahidi kutekeleza maagizo, yote aliyoyatoa lengo likiwa ni kuhakikisha wanafunzi wa kidato cha kwanza wanapangiwa na kuanza masomo mapema mwezi Januari 2023.

Awali Afisa Elimu sekondari, halmashauri ya arusha, Mwl. Menard Lupenza amesema kuwa, Serikali kupitia program ya SEQUIP ilitoa kiasi cha shilingi milioni 470 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari Kiutu, ujenzi unaojumuisha jengo la ghorofa mbili lenye kubeba vyumba 8 vya madarasa, maktaba, maabara za masomo ya TEHAMA na  vyoo vya wanafunzi, jengo la Utawala na Maabara za masomo ya Kemia, Fizikia na Baiolojia.

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa