Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, amekutana na watanzania wazalendo wanaojitolea kufundisha shule ya msingi shikizi Kale, kata ya Ilorienito zaidi ya Km 120 kutoka makao makuu ya wilaya ya Longido.
Shule hiyo ina walimu wanne, mmoja ni mwajiriwa na wengine watatu wa kujitolea, Onding'idi Ndiringo, Tumaini Ngasiaka, Maayani Ngudede wanaofundisha shule hiyo.
Hata hivyo mkuu wa mkoa huyo licha ya kuwashukuru kwa kuonyesha uzalendo mkubwa wa kujitoa kuwagundisha watoto hao bila ajira ya kudumu, amewapongeza kwa kuwapa zawadi ndogo ishara ya kuthamini kazi wanayoifanya amewataka kuleta vyetivyao vya kidato cha nne ili aweze kuwasidia waweze kupata nafasi za kusomea kozi ya ualimu katika vyou hapa nchini.
"Niwapongeze sana, walimu hawa kwa kazi kubwa wanayoifanya ni uzalendo wa hali ya juu, unaopaswa kuigwa na watanzania wote, niwaahidi kama Serikali tutasimamia waweze kupata nafasi ya vyuo vya ualimu wasomee kozi hiyo" Amesema Mhe. Mongella
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa