Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Idd Kimanta, amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Monduli ACP Edward Balele kuwa Wilaya ya Monduli haijawai kupata hati chafu tokea serikali ya awamu ya tano iingie madarakani.
Mheshimiwa Kimanta ameyasema hayo alipokuwa akimkabidhi ofisi Mkuu huyo wa Wilaya katika ofisi za wilaya ya Monduli na kisha kuzungumza na watumishi wa ofisi ya mkuu wa Wilaya na halmashauri.
Amemtaka Mkuu uyo wa Wilaya kuhakikisha hadhi ya Wilaya ya Monduli inabaki kama ilivyo.
“Nakukabidhi Wilaya hii ya Monduli na watumishi wote wakiwa katika hali nzuri na wewe hakikisha unaendelea kufanya nao kazi vizuri na kwa ushirikiano mkubwa”.
Amesema watumishi wa Monduli kwa ujumla ndio waliofanikisha mafanikio yake hadi kufikia nafasi hiyo ya mkuu wa Mkoa, hivyo amewashukuru kwa ushirikiano wao waliouwonesha na kuwataka waendelee hivyo hivyo hata kwa mkuu huyu mpya wa wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mheshimiwa ACP Edward Balele amemuadi Mkuu wa Mkoa kuwa atayaendeleza yale yote ambayo ameyaacha katika wilaya hiyo kwa maendeleo ya wilaya hiyo.
Balele amemuomba Mkuu wa Mkoa kuendelea kuwashauri katika mambo mbalimbali ya wilaya hiyo pale watakapoitaji ushauri wake.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi wote wa Monduli Mkurugenzi wa halmashauri ya Monduli bwana Ulaya Underson, amesema watumishi wote wamefurai sana kwa uteuzi huo na wanamuombea mafanikio katika majukumu yake hayo mapya.
Amesema Kimata ameacha alama kubwa na nzuri sana katika wilaya hiyo na kuaidi kuyaendeleza yale waliyoweza kujifunza kutoka kwake huku wakishirikiana na Mkuu mpya wa wilaya.
Mheshimiwa Kimanta amekabidhi ofisi yake ya zamani ya wilaya kwa mkuu mpya wa wilaya hiyo baada ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha mapema wiki hii.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa