Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Idd Hassan Kimanta, ameishauri Bodi ya shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kutoa huduma illiyo bora kwa wananchi na mapema.
Ameyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo kwa wakurugenzi wa bodi ya TANESCO, Jijini Arusha.
Pia, amewashauri mafunzo hayo wanayoyapata wayafikishe hadi ngazi za chini katika shirika hilo,hiyo itasaidia wote kuwa na mtazamo mmoja na itawaongezea nguvu ya kufanya kazi kwa ushirikiano huku wakivumiliana.
Akitoa neno la shukrani Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umeme Tanzania Dkt. Tito Mwinuka, amesema nasaa zote zilizotolewa na Mhe. Kimanta ni maelekezo kwao kwa ajili ya utekelezaji.
Dkt. Mwinuka amesema,kama bodi watahakikisha TANESCO inatoa huduma iliyo bora na rafiki kwa wananchi wote.
Bodi ya wakurugenzi wa shirika la umeme Tanzania,inafanya mafunzo ya siku 3 jijini Arusha kwa lengo la kuona namna ya kutoa huduma iliyo bora ya usambazaji wa umeme nchini.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa