Leo Jumanne Novemba 19, 2024 kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano AICC, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amekutana na Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini, akisisitiza umuhimu wa kulinda amani na utulivu katika kipindi hiki cha Kampeni za Uchaguzi wa serikali za mitaa.
Mhe. Makonda amesema amani na utulivu unaoshuhudiwa Mkoani hapa umekuwa muhimu katika kuchochea shughuli mbalimbali za kiuchumi, ikiwemo kusaidia Ongezeko kubwa la tija za kiuchumi zinazotokana na mnyororo mzima wa thamani katika sekta ya Utalii mkoani Arusha.
Awali katika hotuba yake kando ya kumshukuru Rais Samia kwa hatua za kimaendeleo zinazopigwa Mkoani Arusha, Mhe. Makonda amewasilisha pia salamu za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Viongozi hao wa dini, akisema Rais Samia anatambua na kuenzi mchango wa viongozi hao wa dini kwani mafunzo na maonyo yao yamekuwa sehemu ya kuwafanya wananchi kuwa watiifu na waaminifu katika kuishika sheria ya nchi na kuhofia kujihusisha na maovu.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa