Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Paul Christian Makonda amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama Mkoani humo kwa namna ambavyo vinaimarisha ulinzi na usalama wakati wote bila kuchoka.
Mkuu huyo wa Mkoa ametoa pongezi hizo leo Machi 01,2025 wakati akiongea na maafisa na askari wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kumaliza mazoezi ya kutembea (route Match) katika barabara mbalimbali za Jiji la Arusha
Mheshimiwa Makonda Pamoja na kuvipongeza vyombo hivyo vya ulinzi na Usalama, Pia ametumia fursa hiyo kuwaarika maafisa hao na askari katika shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo yanafanyika kitaifa Mkoani Arusha kuanzia leo machi 01 hadi tarehe 08, 2025.
Nao wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama Mkoani humo kwa Pamoja wamewataka maafisa na askari kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara kwani pamoja na kuimarisha afya za miili yao pia yanajenga ushrikiano mzuri miongoni mwao.
Copyright ©2017 Arusha Regional Comissioner's Office. All rights reserved.