Msanii Papychuno kutoka Mkoani Arusha ni miongoni mwa wenyeji wa Mkoa wa Arusha waliopata fursa ya kupanda kwenye Jukwaa la Churchil in Tanzania jana Jumamosi Disemba 28, 2024 kwenye kituo cha mikutano AICC.
Papychuno ametokana na Usahili (Audition) iliyofanyika siku ya Christmas, ikisimamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda na Uongozi wa Churchil show kwa kushirikiana na baadhi ya wasanii wakongwe wa vichekesho kutoka nchini Kenya.
Papychuno licha ya kuwa kipaji chake ni kuimba, alipata fursa ya kutumbuiza jukwaani na kutokana na changamoto alizonazo, Alibahatika kuwezeshwa baadhi ya mahitaji yake ikiwemo kusaidiwa kurekodi nyimbo zake, kulipiwa kodi, kurejeshewa meno ya bandia kutokana na meno yake kadhaa kung'oka wakati wa ajali aliyoipata, sambamba na mahitaji mengineyo.
Misaada hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Paul Christian Makonda, Pastor Tony Kapola, Uongozi wa Church show pamoja na wadau wengine kutoka nchini Kenya.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa