Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda, ametangaza kuanza kwa ziara ya kikazi ya siku 6 ya ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Jemadari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Kufanya Mikutano ya Hadhara kwenye halmashauri sita za Mkao wa Arusha.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Magari ya Jeshi la Zimamoto na Ukoaji Mkoani Arusha, Mhe. Makonda amesema katika mikutano ya hadhara atasikiliza na kupokea kero za wananchi wa maeneo hayo ja kuwataka Watendaji wa ngazi zote kuanzia ngazi ya Mtaa/ kitongoji, Kijiji, Kata, halmashari, Wilaya hadi Mkoa kujiandaa ipasavyo kuwa na majibu ya kero hizo na kueleza kuwa, hatovumilia uzembe, ubadhirifu ama kusuasua kwa miradi ya maendeleo kunakofanywa kwa makusudi na baadhi ya watendaji.
Mhe. Mkuu wa mkoa amewasisitiza wananchi wote wa mkoa wa Arsuha kuhudhuri Mikutano hiyo ya Hadhara katika halmashauri zao kwa tarehe zilizopangwa ili kuweza kuzungumza pamoja na wenye kero kuziwasilisha kupitia mikutano hiyo huki akendelea kuahidi kuwa wananchi wote walodhulumiwa haki zao atahakikisha wanarejeshewa.
"Mkoa wa Arusha unatakiwa kuwa namba moja katika usimamizi wa haki, kupiga vita vitendo vya rushwa, dawa za kulevya pamoja na kuwa kinara katika uwajibikaji na kuwa nguzo kuu ya watendaji wote wa mkoa wa Arusha.
Ziara hiyo itaanza rasmi siku ya Alhamisi ya Mei 23, 2024 katika wilayani Longido kabla ya kuelekea Halmashauri ya Karatu Mei 24, Monduli Mei 25, Mei 28 halmashauri ya Arusha, halmasahuri ya Meru Mei 29, 2024 na hitimisho la siku zake sita litakuwa kwenye Jiji la Arusha tarehe 30, Mei 2024.
Mhe. Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano yake ya hadhara na kuja kusema kuhusu haki zao zilizoporwa ama kuhusu watendaji wasiowajibika kikamilifu katika kumsaidia majukumu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa