Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K Mongella amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bweni la wavulana shule ya Sekondari Kitumbeini, kijiji cha Lopolosek, wilaya ya Longido na kuwasisitiza kuongeza kasi iya ujenzi ili likamilike na kuanza kutumika.
Mhe. Mongella amemuagiza Mkuu wa wilaya hiyo, kusimamia mafundi usiku na mchana ili waongeze kasi ya ujenzi na liweze kukamilika, ili lianze kutumiwa na wanafunzi hao, wenye uhitaji mkubwa, kulingana na idadi kubwa ya wanafunzi shuleni hapo.
Mradi huo wa bweni unatakelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF, OPEC awamu ya IV, kwa gharama ya shilingi milioni 155.4, bweni ambalo linategemea kukamilika mwishoni mwa mwezi Februari, 2024.
Mkuu wa shule hiyo, Mwl. ameweka wazi kuwa, lengo la ujenzi wa bweni hilo ni kuwezesha upatikanaji wa malazi bora kwa wanafunzi ili kurahisisha tendo la kujifunza na kufundisha kwa walimu na wanafunzi hasa kwa kuzingatia mazingira rafiki kwa wanafunzi hupandisha taaluma na kuongeza kasi ya ufaulu.
Hata hivyo wananchi wa Kijiji cha Lopolosek ilipo shule hiyo, wameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuona umuhimu wa kujenga bweni hilo la wavulana, litakalosaidia watoto wao kupata elimu bora, kwa kulala shuleni tofauti na wanapolala nyumbani, ambapo hulazimika kutembea umbali mrefu kwenda na kurudi shuleni.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Msimamizi wa mradi huo, gazi ya jamii, Isaya Laizer, amesema kuwa, kutokana na mazingira hatarishi ya eneo hilo wanafunzi wote hulazimikq kulala shuleni, hivyo bweni hilo ni muhimu kwa watoto hao, kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaopangiwa shuleni hapo na kusababisha shule kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi kila mwaka.
"Tunamshukuru rais wetu, mama Samia kwa kazi nzuri anayoifanya, tunamuombea afya njema ili aendelee kuwatumikia watanzania, kwa kipindi kifupi amefanya kazi kubwa inauoonekana, Kitumbeini ni mbali mwisho wa dunia, tulisahaulika kwa miaka mingi lakini awamu hii ya sita, kila pesa zinakuja kila kona ni maendeleo ya Mama Samia" Amebainisha Leskari Loserian Laizer
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa