Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K Mongella, ametoa msaada wa vyakula kwa watoto yatima, kwenye makazi ya 'The Joy of God Ophanance' ya Jijini Arusha, kupitia fedha walizozawadiwa na watumishi wa Sekretariet mkoa wa Arusha, wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa 2024.
Mhe. Mongella ametimiza ahadi yake Februari 02, 2024, aliyoitoa siku ya sherehe ya kukaribisha mwaka 2024, baada ya watumishi wa Sekretariet mkoa wa Arusha, kuwazawadia fedha yeye na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Missaile Albano Musa pamoja na Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu, David Francis Lyamongi, na kuahidi fedha hizo kuzipeleka kwa watoto yatima.
"Tunawashukuru watumishi wote kwa zawadi hii mliyotupatia, tunaithamini sana na kutambua umuhimu wake, lakini fedha hizi tutanunua chakula na kupeleka kwa watoto yatima, Sista wa kituo cha The Joy of God, amenipigia simu kuwa wana uhitaji wa chakula katika kituo hicho" Aliahidi Mhe. Mongella.
Akizungumza mara baada ya kupokea chakula hicho, Msimamizi wa kituo hicho, Sista. Janeth Mosten Ngopa, licha ya kumshukuru sana Mhe. Mongella kwa upendo na huruma yake ya kuwakumbuka na kuwajali watoto yatima, na kusema kuwa, zawadi ya chakula kwa watoto hao ina thamani kuwa, kwa kuwa uwepo wa chakula cha kutosha kituoni, unawakikishia afya watoto hawa pamoja na kuwafanya kuwa na furaha na matumaini kwakati wote.
“Tunamshukuru sana Mhe. Mongella kwa upendo wake kwetu na moyo wake wa kutoa, tunamuombea kwa Mungu azidi kumbariki, kupitia yeye watoto hawa wanafarajika, hata sisi walezi tunakuwa na amani, zaidi sana tunamshuru Mhe. Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan, kwa kutuletea Mhe. Mongella Arusha, kiongozi mwenye upendo wa dhati kwa wananchi wake bila kujali hali zao, amekuwa ni sehemu ya familia katika vituo vya kulelea watoto yatima na wenye uhitaji, hatujawahi kuomba msaada kwake tukakosa, Mungu akubariki sana ”. Amesema Sister Ngopa
Hata hivyo, watoto hao wamemshukuru Mkuu huyo wa Mkoa, kwa kuwajali na kujitoa mara zote bila kuchoka, kwa kuwa amekuwa akiwatembelea mara kwa mara na kuwapa mahitaji tofauti tofauti na kuahidi kuendelea kumuombea baraka kutoka kwa Mungu.
“Kupitia chakula hiki tunamuombea sana mkuu wa mkoa, Mungu ampe maisha marefu na azidi kumbariki kwa kumzidishia mara dufu pale alipotoa kwaajili yetu”. Amesema Dominick Denis.
Awali, vyakula vilivokabidhiwa ni pamoja na Kg 150 za Mchele Kg 65 za unga wa mahindi, Kg 100 na Kg 50 za maharage vyote vikiwa na thamani ya shilingi 822,000.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa