Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K.Mongella amekagua mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Monic wilaya ya Ngorongoro, mradi unaotekelezwa na Serikali kupitia programu ya kuboresha miundombinu ya shule za Msingi Tanzania Bara BOOST.
Akitoa taarifa ya mradi huo, Mwalimu Mkuu shule ya Msinhi Monic, Mwl. Olosotun Masiaya amesema kuwa mradi huo umetekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 105.8, ikujumuisha ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na matunzu ya vyoo, ukiwa ni muhimu kwa kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani kama ilivyokuwa hapo awali.
Amesema kuwa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 878, wasichana 330 na wavulana 548 huku wanafunzi 477 wakiwa ni wanafunzi wa bweni kutokana na mazingira ya eneo hilo.
Aidha Mwl. Masiaya ameishukuru serikali a awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu ya elimu nchi, miundombinu ambayo ni rafiki kwa kufundishia na kujifunzia kwa walimu na wanafunzi, mazingira ambayo yanarahisisha uhawilishaji wa ujuzi na maarifa kwa wanafunzi darasani.
"Miundombi hii rafiki inatusaidia hata sisi walimu kufundisha kwa kuwafikia mwanafunzi mmoja mmoja, kutokana na idadi ndogo ya wanafunzi,tofauti na darasa likiwa na mrundikano wa wanafunzi ufundishaji unakuwa mgumu"Amebainisha Mwl. Masiaya.
#MamaSamiaAnairushaArusha
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa