• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Arusha Regional

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia ya Mkoa
      • Chimbuko/Asili ya eneo
      • Orodha ya wakuu wa Mikoa
    • Dira na dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji Mali
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Wilaya
    • Arusha
      • Historia
      • Viongozi
    • Arumeru
      • Historia
      • Viongozi
    • Monduli
      • Historia
      • Viongozi
    • Karatu
      • Historia
      • Viongozi
    • Longido
      • Historia
      • Viongozi
    • Ngorongoro
      • Historia
      • Viongozi
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Arusha
    • Halmashauri ya Arusha
    • Halmashauri ya Meru
    • Halmashauri ya Monduli
    • Halmashauri ya Karatu
    • Halmashauri ya Longido
    • Halmashauri ya Ngorongoro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Ardhi
    • Utalii
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Picha Mbalimbali
    • Habari
    • Matukio

RC MONGELLA AWAONGOZA WAKAZI WA ARUSHA KUADHIMISHA SIKU YA UKIMWI DUNIANI 2023..

Posted on: December 1st, 2023

Na Elinipa Lupembe


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John V.K. Mongella, amewaongoza wakazi wa mkoa wa Arusha, kuadhimisha Siku ya UKIMWI DUNIANI 2023, Desemba 1, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mazingira Bora wilaya ya Karatu.


Mheshimiwa Mongella, amewataka wananchi kushiriki katika kutokomeza UKIMWI, kwa kuhakikisha kila mmoja anajilinda na kumlinda mweingine kwa afya na maendeleo ya jamii na Taifa.


Amesema kuwa, maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani, yanaikumbusha dunia kujihadhari na ugonjwa huo pamoja na kuunga mkono juhudi za mashujaa, watalamu, ndugu, jamaa na marafiki, walipoteza maisha kutokana na Ugonjwa wa UKIMWI.


Ameongeza kuwa, siku hii muhimu imkumbushe kila mtu kupima na kujua afya yake na pale anapogundulika ameathirika, apate ushauri na kuanza kutumia dawa za kufubaza UKIMWI


Ameweka wazi kuwa, Serikali ya awamu ya sita imewekeza fedha nyingi, kwenye sekta ya Afya hususani katika utoaji na upatikanaji wa huduma za Virusi vya UKIMWI na UKIMWI kwa kutoa bure, Dawa za kufubaza Virusi vya UKIMWI, ili waathirika waweze kupata muda wa kuishi na kufanya kazi kwa maendeleo yao binafsi na taifa lao.


Mratibu wa UKIMWI, Magonjwa ya ngono na Homa ya Ini mkoa wa Arusha, Dkt. Haika Ernest Mhando, amesema kuwa, kulingana na tafiti ya mwaka 2017 - 2016, hali ya maambukizi kwa mkoa wa Arusha ni asilimia 1.9,  na kwa kipindi cha Januari mpaka Novemba 2023, jumla ya watu 1,253,000,  walijitokeza kupima maambukizi ya VVU.


Amefafanua kuwa, kati ya hao, watu 3,586  walikutwa na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI sawa na  2.8 % , wanaume ni 2.4% na wanawake  ni 2.9%, huku wote wanaendelea kupata huduma katika vituo mbalimbali vya afya ndani ya mkoa wa Arusha.


Hata hivyo wana Konga Karatu, wameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwahudumia wathirika kwa kuwapa dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI, dawa ambazo zinasaidia waathirika kuishi muda mrefu na kujitegemea kwa kufanya kazi za kulijenga Taifa na kujipatia kipato kwa maendeleo ya Taifa.


"Mimi nilizaliwa na Virusi vya UKIMWI, lakini uwepo wa dawa za kufubaza virusi, zimenisaidia ninaishi mpaka leo kwa amani, nikitekeleza kazi zangu kama watu wengine" Amesema Emmanuel Fransisca


Awali, Katika Maadhimisho hayo Mkuu wa mkoa huyo, ametembelea mabanda ya maonesho ya afya, wajasiriamali wadogo, na TAKUKURU, yaliyohimiza upimaji wa afya, Ushauri Nasaha na matumizi ya Dawa za kufubaza Virusi vya UKIMWI kwa maendeleo ya jamii na Taifa.


Kauli Mbiu : Jamii Iongoze, Kutokomeza UKIMWI.

Tangazo

  • TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA MOCK MKOA DARASA LA SABA 1 July 06, 2023
  • MATOKEO YA MOCK MKOA DARASA LA SABA 2 July 07, 2023
  • TAZAMA MATOKEO YA MOCK MKOA KIDATO CHA NNE July 07, 2023
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • RC MAKONDA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA YA ESO - LONGDON NA UKUMBI WA MIKUTANO ARUSHA.

    April 03, 2025
  • RC MAKONDA ATAKA KUPEWA MAJINA YA WATENDAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO YA KIJAMII.

    March 28, 2025
  • KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA NI MAONO NA MAELEKEZO YA RAIS SAMIA- WAZIRI NDUMBARO.

    March 28, 2025
  • OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI YAFANYIA KAZI MALALAMIKO WANANCHI WA MIANZINI ARUSHA.

    March 28, 2025
  • Angalia Zote

Video

UZINDUZI WA BARABARA YA WASO-SALE
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • SALARY SLIP
  • Taarifa ya Mapato
  • Taarifa za Shule (SIS)
  • Takwimu za Sekta ya Elimu (BEMIS)
  • Video

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Portal ya Watumishi
  • Takwimu
  • TANAPA

Watembeleaji

world map hits counter

Wasiliana Nasi

Mawaliliano mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani
    • Maswali ya Mara kwa Mara

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa