Na Elinipa Lupembe
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella, ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa miundombinu ya shule ya sekondari ya kata ya Sekei, mradi unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 584.2 fedha kutoka Serikali Kuu.
Mkuu huyu wa mkoa ameushauri uongozi wa Jiji la Arusha kujipanga kujenga majengo ya ghorafa, hali inayotokana na ufinyu wa ardhi katika jiji hilo ili kuwapa nafasi wanafunzi kufanya shughuli nyingine za mitaala ya nje kama michezo, kilimo na ufugaji.
Amesema kuwa licha ya kuwa serikali inawekeza miundombinu na kuweka mkazo kwenye taaluma, inapaswa kuzingatia ukuaji wa mtoto unaendana na muasuala ya kijamii ili aweze kukua kiakili, kimwili ja kisaikolojia.
" Ninaishukuru serikali awamu ya sita imetoa fedha nyingi za kutekeleza miradi ya elimu ili kuhakikisha watoto wote wa kitanzania wanapata elimu kwenye mazingira bora na rafiki lakini zaidi kila mtoto mwenye uri wa kwenda shule awe shuleni kwa kutoa elimu bila malipo, inayowawezesha hata watoto wanaotoka kwenye familia zenye kipato cha chini wanakwenda shule bila kizuizi cha kushindwa kumudu gahrama" Amesema
Naye Diwani wa kata ya Sekei Mhe. Gerald Sebastian ameishukur serikali ya awamu ya sita kwa kuleta fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya kata, kata ambayo haikuwahi kuwa na shule kama ilivyo kwa kaya nyingine
"Kwa niaba ya wananchi wa Sekei tunamshukuru mheshimiwa Rais kwa kuwaonea imani wananchi wa kata yetu kata ambayo ian idadi kubwa ya wananchi lakini haikiwa na shule ya sekondari watoto wetu zasa watasoma nyumbani, kuhusu nafasi tutajipanga kuanza kujenga majengo ya kwenda juu ili kumeneji matumizi bora ya ardhi.
Naye msimamizi wa mradi huo mkuu wa shule mama ya sekondari Kimaseki, Mwl. Joseph Manase Maro amesema kuwa jumlamya wanafunzi 80 wa kidato cha kwanza wanatarajiwa kupangiwa shule hiyo kwa mwaka wa masomo utakaoanza Januari 2024 na kuonheza kuwa watapata nafasi ya kusoma katika majengo mazuri na ya kisasa na kupunguza adha ya kutembea umabli mrefu kwenda na kurudi shuleni.
#ARUSHAFURSALUKUKI
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa