Na Prisca Libaga Arusha
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amesema sekta ya Maendeleo ya Jamii ni daraja wezeshi katika kuwainua wananchi kiuchumi na hivyo Serikali imeandaa mpango wa maendeleo kupitia sekta hiyo ya maendeleo ya jamii katika kutokomeza Umaskini na Ukatilli wa Kijisia kwenye Jamii kwa kutumia rasilimali zilizopo kwenye jamii yenyewe.
Waziri Gwajima amelitumia Kongamano la 16 la Mwaka la Wataalamu wa Maendeleo ya jamii nchini linalofanyika kwa siku tatu jijini Arusha kuwaeleza wataalamu hao wa Maendeleo ya Jamii umuhimu wa kuwaelimisha na kuwafikia wananchi wa ngazi ya chini vijiji na vitongoji juu ya fursa mbali mbali zinazotolewa na Serikali
Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstafu Mizengo Petter Pinda anapendekeza kwa Serikali kuitazama kwa jicho la pekee sekta hiyo kwa kutoa nyenzo muhimu kwa watalamu hao ili wajikite katika kutatua kero za maendeleo ya Jamii hasa katika ngazi ya vijijini.
Awali Naibu katibu Mkuu Wizara wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju ameeleza kaulimbiu ya mwaka huu “Ni Sekta ya Maendeleo ya Jamii:Msingi imara wa uwezeshaji Wananchi.
Awali Waziri Gwajima ametembelea Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru(TICD) ambayo inaadhimisha miaka 60 ya kuanzishwa kwake. Bakari George ni mkuu wa taasisi hiyo anaeleza mchango wa taasisi hiyo kwa Taifa
Mwisho.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa