Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) ameeleza kuwa, sekta ya Uhasibu ina mchango muhimu katika kuimarisha usimamizi bora wa fedha, na inatoa mwanga wa matumaini kwa juhudi za pamoja za kujenga msingi imara kwa maendeleo endelevu ya Bara la Afrika.
Mhe. Mwigulu amesema hayo, wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi, Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa Innocent L Bashungwa kufungua rasmi Mkutano wa Pili wa Jumuiya ya Wahasibu Wakuu wa Serikali wa Nchi za Afrika kwa niaba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), ambao umewakutanisha wadau zaidi ya 2000 kutoka ndani na nje ya bara la Afrika.
Aidha, alitumia fursa hiyo kuwaeleza washiriki wa Mkutano huo, hatua muhimu ambazo Serikali imezichukua katika kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ukiwemo, ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, ujenzi wa madaraja, na miradi mingine ya kijamii.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa