Na Elinipa Lupembe
Imeelezwa kuwa, Serikali ya awamu ya sita, chini ya uongozi wa Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanya mapinduzi makubwa ya maendeleo katika seka zote, kisiasa, kiuchumi na kijamii, maendeleo ambayo yamewagusa wananchi moja kwa moja katika maeneo yao.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Deogratius Ndejembi, wakati akizungumza kwenye Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei mosi, iliyofanyika kitaifa mkoa wa Arusha, kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Mei 01, 2024.
Mhe.Ndejembi, amesema kuwa, kila mtanzania ameshuhudia maendeleo makubwa kwenye sekta zote kisiasa, kiuchumi na kijamii, bila kuwacha nyumma wafanyakazi, kukiwa na ongezeko kubwa la ajira mpya zinazoendelea kutangazwa, kupanda kwa madaraja, nyongeza za mishahara na mazingira ya kufanyia kazi yakiendelea kuboreshwa.
"Mheshimiwa Makamu wa Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu yenye dhamana ya kazi, itaendelea kuimarisha utatu kwa kushirikiana na vyama vya wafanyakazi na waajiri katika kusimamia utekelezaji wa sheria, kanuni na taratibu za kazi kwa lengo la kuimarisha mahusiano mema mahala pa kazi". Amesema Mhe. Ndejembi
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa