Sekretarieti ya Mkoa wa Arusha imeagizwa ndani ya mwezi mmoja kuzitambua na kuketi pamoja na asasi na mashirika ya binafsi yasioingiza faida ili kupanga mkakati wa pamoja wa kuona namna ambavyo watakuza ufanisi katika kuhudumia wananchi wa mkoa wa Arusha.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda wakati alipokutana na wadau wa asasi na mashirika hayo ya kiraia, ikiwa ni miongoni mwa maazimio yaliyofikiwa na kikao hicho katika kukuza ufanisi na kuimarisha utendaji kazi wa taasisi hizo muhimu kwa maendeleo ya Mkoa wa Arusha.
Katika hatua nyingine pia Mkuu wa Mkoa ameunda kamati ndogo inayotokana na wajumbe kutoka kwenye asasi na mashirika hayo, kwaajili ya kupitia na kuchambua sheria na kanuni mbalimbali ambazo zimekuwa zikisababisha mgongano na vikwazo kwenye utendaji wa asasi na mashirika yanayofanya kazi mkoani Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema mapendekezo yatakayotokana na uchambuzi huo yatawasilishwa kwa Mamlaka husika lengo likiwa ni kupata sera na sheria ambazo zitakuwa rafiki kwa asasi na mashirika hayo pamoja na kwa wafadhili wanaosaidia asasi na mashirika hayo kufanya kazi zake.

Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa