Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa umoja wa Mabunge duniani IPU Dkt. Tulia Ackson akihutubia kwenye Mkutano wa 53 wa Chama Cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola kanda ta Afrika,amewataka washiriki wa Mkutano huo kutumia Jukwaa hilo vyema katika kuunda ushirikiano imara zaidi, kubadilishana mawazo bunifu na kuendeleza mikakati inayoweza kutekelezeka ambayo itakuwa na manufaa kwa bara la Afrika.
Dkt. Tulia Ackson ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Oktoba 03, 2024 wakati wa ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika Kwenye Ukumbi wa Grand Malie Jijini Arusha, Mkutano unaofunguliwa na Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango na kuhudhuriwa na washiriki kutoka nchi zaidi ya 19 kutoka Barani Afrika.
Spika Dkt. Tulia ametumia fursa hiyo pia kuwashukuru wajumbe wa Mkutano huo kwa kumchagua Kuwa Rais wa Mabunge duniani, akiwahimiza pia kutumia uwepo wao Mkoani Arusha kuweza kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii vinavyopatikana mkoani hapa.
Hatimiliki ©2018 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Haki Zote Zimehifadhiwa